Posts

recently

Magufuli ateua maprofesa watatu kuongoza taasisi

Image
8, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 18 Agosti, 2017 amefanya uteuzi wa viongozi wafuatao; Kwanza, Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Abdulkarim Hamis Mruma kuwa Mwenyekiti wa Kampuni ya Kuhifadhi Mafuta (TIPER). Prof. Abdulkarim Hamis Mruma ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania. Pili, Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Joseph Buchweshaija kuwa Mwenyekiti wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania Ltd. Prof. Joseph Buchweshaija ni Naibu Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE).   Tatu, Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Evaristo Joseph Liwa kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ardhi (Ardhi University).   Prof. Evaristo Joseph Liwa amechukua nafasi ya Prof. Idrissa B. Mshoro ambaye amestaafu.   Uteuzi wa viongozi hao umeanza tarehe 17 Agosti, 2017 Emmanuel Buhohela Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi Dar es Salaam 18 Agosti, 2017

TID aikana mimba ya Rachel

Image
TID aikana mimba ya Rachel Msanii Khalid Mohamed maarufu kwa jina la TID, ameruka viunzi na kukana tetesi za kumpachika ujauzito msanii mwenzake Rachel. Akizungumza kwenye kipindi che eNewz kinachorushwa na East Africa Television, T. I. D amesema kwa sasa hatarajii mtoto yeyote na mwanamke yeyote, na kwamba habari hizo hazina ukweli. “Hapana, sitarajii mtoto yeyote na Rachel, sina mimba ya Rachel, siyo kweli bwana, hamna mtu mwenye mimba wala nini, kila mtu anataka kuwa na mimba ya Mnyama, sasa wanawake wangapi wanataka kuwa na ujauzito wa mtoto wangu?”, alisikika T. I. D Hivi karibuni kulikuwa na tetesi kuwa wasanii hao wana mahusiano ya kimapenzi, zilizoibua habari kuwa Rachel ana ujauzito wake.
Image
MAGAZETI YA LEO 19/8/2017 Saturday, August 19, 2017  
Image
Mnamo Jumatatu tarehe 21 Agosti, tukio lisilo la kawaida litashuhudiwa Amerika Kaskazini, ambalo limewavutia watu zaidi ya milioni saba wanaotarajia kulishuhudia katika miji mbalimbali Marekani. Kwa mara ya kwanza tangu 1918, jua litapatwa kikamilifu na mwezi Marekani. Bara lote la Amerika Kaskazini litafunikwa na giza totoro mchana, Ingawa baadhi ya watu wanalitazama tu kama tukio la kuvutia, kwa wengine, hili linaashiria mwisho wa dunia kama tunavyoifahamu kwa sasa. Makundi mbalimbali ya Kiinjilisti nchini Marekani kwa mfano, yameanza kuhubiri kwamba tukio hilo linaashiria kukaribia kwa mwisho wa dunia. Tovuti moja ya unabii wa Kikristo kwa jina Unsealed imedai kwamba tukio hilo la Jumatatu litaanzisha kipindi cha Majonzi, kipindi cha miaka saba ambapo katika kipindi hicho asilimia 75 ya watu wote duniani wataangamizwa. Kwa wengine hata hivyo, ni tukio ambalo wamesubiri sana kwa hamu majira haya ya joto. Kuna watu 12 milioni ambao wanaishi eneo la upana wa maili 70 9kilomit...